Late yesterday the “Dowans Saga” came to what some may consider its most logical conclusion.
For those who are unfamiliar with this saga… Hawa Dowans ndio walionunua na kupokea mikoba ya kampuni hewa Richmond. Baada ya kusuasua kwa miezi/miaka kadhaa, na kushindwa kabisa kutimiza wajibu wao TANESCO waliamua kuvunja mkataba wao na hawa jamaa (na kukomboa mamilioni "kazaa" ambayo hawa jamaa walikuwa waki ya chuna kiulaini). Jamaa waliamua kufungua kesi mahakamani – Aidha Dowans pia wakatangaza nia yao ya kuuza mitambo yao iliyopo Tanzania (ambayo ilikuwa imeshatumika – yaani si mipya). TANESCO kwa kuchelea kutiwa “changa la macho” (na hasa kwa kuwa walikuwa wanawadai hawa jamaa wa Dowans "kitu kidogo") waliamua kufungua kesi kuzuia uuzaji wa mitambo hiyo. Ni muhimu kufahamu kuwa kesi zote hizi mbili bado zipo mahakamani (naomba kurekebishwa iwapo moja ilisha kwisha).
round hii ya hili saga ilianza pale TANESCO ilipotaka kununua mitambo hiyo ya Dowans (ambayo si mipya) kwa kutoa sababu kuwa “ina ihitaji ili kuzuia giza kubwa linaloweza kuigubika nchi yetu hapo baadaye - december…”
Kisheria… (Public Procurement Act) ni marufuku kwa serikali au shirika lolote la kiserikali kununua mitambo ambayo imeshatumika (kama ilivyo ya Dowans). Kamati ya bunge ya nishati na madini (ikiongozwa na Mhe. Shelukindo) ililiona hilo na kushauri TANESCO (neno kushauri ni key hapa) kufuta mpango wake wa kununua mitambo hiyo ya Dowans, na badala yake mipango ifanywe, tenda itangazwe na inunuliwe mitambo "mipya" - hata kama hilo litamaanisha kuongeza pesa kidogo. In my humble opinion... a very good and professional ushauri! Hasa kwa kuwa bei inayoongelewa ili kuweza kununu mitambo ya Dowans ni 75% ya bei ya kuweza kupata mitambo ambayo ni "Brand new".
TANESCO wakaona haiwezekani... wakaamua kuwakilisha kesi yao kwa kamati nyingine ya Bunge (Mahesabu na uhakiki wa mashirika ya umma - iunayoongozwa na Mhe. Zitto Kabwe). Somehow wao (kamati ya Mhe. Zitto Kabwe) wakaridhia TANESCO wanunue mitambo hiyo… sababu iliyotolewa “...ili kulinusuru taifa kutokana na giza linalokuja..." neno "national Interest" pia lilitumika.
Just like that kukawa na kamati mbili za bunge zinapingana na kutupiana madongo “mbere ya ru-public”– a perfect recipe for public humiliation (or was it discussion?)
Nionavyo:
1. Mitambo ni michakavu… the deal should have stoped there!… game over! Unless sheria ina vunjwa au kupindwa… there is no way this deal could go through. Waheshimiwa wote wanalijua hilo (ambao wana jukumu la kuhakikisha sheria zote za nchi - ikiwa ni pamoja na za manunuzi; zinafuatwa). Kwa nini baadhi yao walidhani it is OK kupinda sheria hii ya manunuzi kwa faida ya TANESCO - That is anyone’s guess! Ukweli ni kuwa wengi hatuelewe, na huenda Ingetusaidia sanakama taifa iwapo wenye”nchi” tungeelimishwa ulazima huo umetoka au ulikuwa unatoka wapi.
2. Tulijengewa mazingira ya kuamini kuwa Dowans & TANESCO ni kama panya na paka… na hiyo ikadhihirishwa kwa TANESCO & Dowans kuburuzana mahakamani… Kesi hiyo bado ipo mahakamani na hukumu is still out there. Leo TANESCO na Dowans wanataka kuingia deal mpya… WHAT? Hii ni kweli au "changa la macho tena?... inakuwa kama mtu anasema.... Oh yeah… we in court for a formal dissolution of our former marriage… but Hey what the heck… lets get engage and marry each other all over again…. (???mhh!$@!@%????) - for the rest of us... = kizunguzungu!
3. Board ya TANESCO tayari ilishapinga mpango huu, Speaker ametoa onyo kuhusu hatari ya kuendelea na mpango huu, kamati ya nishati na madini (ambayo ndio husika katika maswala kama haya) nayo pia imepinga … Na watu wengine kadhaa wamepinga.... Kwa maneno mengine… unless mtu unataka kujikaanga (literally)… this deal is dead
OK… hiyo jana alasiri; Mhe. Dr Mkurugenzi akatangaza kuwa; TANESCO wameamua kufuta uamuzi wao huo… lakini pia hakuishia hapo... Mhe. Dr. mkurugenzi akaamua kutoa what may amount to vitisho,.. na hapa ndipo ninapoona inakuwa issue.
Mh. Dr. Mkurugenzi anasema.. Eti “… wameamua kufuta uamuzi wao wa kununua mitambo ya Dowans; lakini taifa litakapo gubikwa na giza hapo december - taifa lijilaumu lenyewe kwa kushindwa kufanya mamuzi na kuwa wao TANESCO hawatakuwa wa kulaumiwa…” mhh????
1. Mhe. taifa ni nani? na TANESCO ni ya nani? mhhh????
2. Mhe. Your job is to get that “juice” to all of our offices, factories, homes and even our cowsheds! You are TANESCO…Tanzania Electric Supply Company Limited... you are a Tanzanian company WHOLLY owned by the government of the URT.. Your job sir is to SUPPLY enough electric energy to meet (and exceed) our national demand. Hii hadithi ya “usilaumiwe” inatoka wapi?
3. Kumbe unafahamu kuna ukame unakuja… by the way hili swala la ukame si jipya; power rationing si zoezi jipya… everyone knows that! Kama kiongozi vipi usijitayarishe wewe na shirika lako SASA… ili kutupunguzia kero hiyo baadaye? In my book... you just announced to the world kushindwa kwako kutimiza wajibu uliopewa... was that the message you intended for us to get?
4. Mhe. Dr. Unataka kutwambia mitambo chakavu ya Dowans IS THE ONLY solution to this problem?
5. Kuna sheria zinazo izuia TANESCO kununua mitambo chakavu… In my book… that should have been “THE END” of story. Hii kitu ya kujaribu na kutaka kupindapinda sheria… inaleta wasiwasi… unajua "waswazi" (waswahili) wanachosema mitaani….I mean kuhusu uwezekano wa uwepo kwa “mkono wa mtu” katika umasikini tulionao? Au pia kuhusu deal hii kuwa ni sehemu ya mchakato wa kujenga “mazingira ya Rushwa” ... yanasemwa mengi... Lakini Mzee wetu mstahiki Dr. huoni statement zako hizi zinatuweka mkao wa kukufikiria vibaya? I mean… come-on- man!!! Were you serious? Kwa sababu hata mtoto mdogo anaweza kufikiria, mzee unaji-set ili kuwepo giza, kisha waswazi tuhahe kutafuta mitambo ya “Emergency”… si ndivyo ilivyo chezwa wakati wa Richmond? Au this is a different play? –from the same play book?
Peace
0 comments:
Post a Comment