Sunday, July 15, 2007

Majukumu na Uwajibikaji

Pamoja na kuwa kuna mchecheto wa Bunge unaoendelea hapa Bongo, swala la kashfa ya benki kuu limeendelea kuchukua kuzito wa juu katika magazeti mbali mbali ya hapa bongo.
Aidha kilichoshangaza kidogo ni ubabe wa mheshimiwa (gavana) wa BOT ambaye baada ya ukimya mrefu aliibuka na kusema kuwa hatajiuzulu kwa kuwa “haoni kosa alilolifanya”
- Swali ni … kuna ugumu gani kwa mzee wetu (gavana) kutambua kuwa “uwajibikaji” si lazima kosa liwe limehakikishwa. Ukweli ni kuwa hata kama yeye bnafsi haku “gandamizaga” hata senti moja! Mtaji wa watu ku-"chomoa" kitu kidogo yeye akiwa kinara, unatosha kabisa kwa yeye japo kuchukua likizo ya kiutawala - ili kutoa nafsi kwa wakaguzi (wa nje) kufanya kazi yao. Kwa kufanya hivyo sio tu angetunza heshima yake, na sifa ya uaminifu ambayo inaonekana ni muhimukwake - bali pia ingesaidia kujenga dhana nzuri ya uwajibikaji katika jamii yetu. badal yake mzee ka“ngangania” na kusema hatoki na kuw ataendelea "kugandamizaga" hadi mwisho… kwa faida ya nani?
- Kwani hakuna utaratibu ambapo ungeruhusu kwa yeye kuji-weka pembeni (japo kwa muda) na iwapo itahakikishwa kuwa madai ni uzushi – ataweza kurudi kazini - only this time akiwa amejikusanyia "equity" zaidi toka kwa wadau? Kwa mtu aliye kwenye nafasi kama yake – that would have been the “gentleman’s” way! Na kwa kweli - zaidi ya "woga" sioni mzee ata-lose nini kwa kujiengua "kuwaachia wakaguzi wafanye vitu vyao. Kwa ku"ngangania" inapelekea kwa baadhi yetu ambao hatuna "inside" information kudhani kuna kitu mzee anaficha"ga"

Peace out!

0 comments: