Tuesday, July 25, 2006

Think Tank - Good or bad Idea?

Kuna wakati niligusia umuhimu wa kujaribu kuanzisha an informal think tank... a group of individual that will be ready to objectively discuss and analyze various issues, policies and events with an intention of influencing future development planning and/or strategies for Tanzania.

Maono (vision) ni ku-provide ideas and information based on "proven" or at a minimal kutoa maoni ambayo yanakubalika katika nyanja (discipline) husika (Industry wide agreed standards)- regardless of the origin.
Of course katika kujadiliana itabidi kuwepo na juhudi za ku-contexualize ideas.. meaning; we should try to avoid wholesome adoption of ideas.

Nionavyo, haiitaji a prophet kuona matatizo katika maamuzi mbali mbali. Ni rahisi mno kuona mapengo au mashimo kwenye policy yoyote ile. LAKINI inahitaji a genius kupata ufumbuzi wa mapengo, mashimo au matatizo yanayotukabili.
Ninaamini itakuwa na faida zaidi iwapo kikundi hiki kitajizatiti kutafuta solutions, na kisha kuhakikisha mawazo hayo yanafika panapohusika.
Yes, ninafahamu kuna watakaoona tunapoteza wakati...; lakini ninaishi marekani, na wakati ambapo "think tanks" ni taasisi zinazokubalika na mara kwa mara kusikilizwa, bado ilichukua muda kufikia hapa walipo - there will always be a learning curve on these things. Aidha tuna REPOA kule nyumbani ambayo kwa maoni yangu wanajitahidi kwa kiasi chao, ingawa sina uhakika kama kuna aliyefanya tathmini ya effective yao katika ku-influence discision makers.

Wakati ambapo huenda tukaanza kwa kujadili policies mbalimbali, ni mategemeo yangu kuwa tutafika mahali quality ya mawazo & ideas zitakazotolewa zitaweza kusaidia our policy makers kupata mtizamo ambao huenda hawakuwa wameufikiria.
Sintashangaa iwapo pia tutafika mahali ambapo tutaweza kuwa na a broad influence to the governing body.
Ninaamini siri yakufanikiwa kwa kikundi kama hiki ni, 1. Ujasiri wa kusema kile kinachofahamika kama ukweli & na haki and 2. Kujikita katika utumishi kwa umma wa waTz rather than to serikali, chama au whatever!

Huduma hii italenga kufamfaidi nani? Who is our client?
= Mtanzania wa kawaida.
YEs... wakati ambapo tunaweza ku-target papers zetu kwa policy makers... kila kitu itabidi kiwe katika kujaribu kuinua hali ya mwananchi wa kawaida.

Means of Dissermination
- White/policy papers, detailed reports to support OR contradict an idea or policy

Why I believe this is doable:
- I believe, kuna watanzania wengi... sehemu mbali mbali duniani, wenye ujuzi na skills tofuati.
- Itakuwa rahisi ku-address different issues ambapo waTz mbali mbali na waatajaribu kutushirikisha maoni kutokana na ujuzi wao.
- I believe by and large wengi wapo tayari kuchangia japo mawazo jinsi ambavyo tunaweza kujikwamua kutokana na umaskini ambao kwa kweli - unaweza kabisa kufutika!

Of course we will need to addressed some dynamics, situations and/or conditions before this idea becomes a reality.
Kwa wakati huu however, lengo ni kujaribu kupima response..., pia kuweza kupata nafasi ya kusoma maoni, mapendekezo etc; kabla hatujapiga hatua nyingine.

Iwapo, unadhani itatusadia, jaribu kuwashirikisha waBongo wengine... popote pale walipo, na bila kujali field zao. Hili bado ni wazo...kama itadhihirika kuwa halifai, no big deal... We will drop everything and move on! But I really believe we need to start thinking on what we can do to change things (to be pro-active - rather that being re-active).

What do you think? Is this idea too idealistic? / do-able?

My senti mbili...talk to me with yours:)
Ned

Thursday, July 20, 2006

$2-a-day job to fight Poverty in Tz?

Katika gazeti la "The New York Times" la jumapili iliyopita (july 16), mwandishi - Daniel Gross alimnukuu MS. Jacqueline Novogratz (mmojawapo wa vingunge wa Rockfellar foundation na mshauri wa Bank ya dunia) akisifia kiwanda cha A - Z kilichopo Arusha kama mfano wa kuigwa katika juhudi za kuondoa umasikini. Unaweza kusoma taarifa hiyo hapa

Inasemekana, baada ya kupata mkopo wa $350,000 (420million Tsh), toka kwa mfadhili wa huku US, kiwanda hicho kimeajiri takribani wanawake 2000 ambao kinawalipa kama $1.80 kwa siku kuzalisha vyandarua vyenye dawa. Mama huyo alisikika akifagilia A-Z kama mfano wa kuigwa kuondoa umasikini...

Swali langu ni... unakubaliana na analysis yake?

Hebu tujaribu kupiga vi-namba kidogo!
Assuming kuwa watu hawa watafanya kazi kwa siku kama 23 kwa mwezi, $1.80 kwa siku inakupa kama $41.4 kwa mwezi. Ukichukulia wastani wa x-change rate ya TSh 1200/= kwa $, wakina mama hawa wanapata kama TSh 49,680/= kwa mwezi.
Kima cha chini Tz ni Tsh 45,000/= kwa mwezi (nirekebisheni kama nimekosea), na wengi "walioajiriwa" wanapata zaidi ya hiyo mara kadhaa!

Kwa upande mwingine...A-Z inasaidia! Inasemekana kuwa Tz pamoja na kuwa na a workforce of about 19.22 million people, ina unemployment rate ya kama asilimia 36 (36%)... yaani takribani watu 6.9 million (ambao wana uweao wa kufanya kazi) hawana kazi! A-Z inaajiri watu 2000 (0.03% ya wasio na kazi... kidogo lakini do hivyo; "chururu si ndo ndo ndo":)

Swali langu ni... unadhani katika rate ya $1.80 kwa siku tutafika? Au ndo hivyo tena... "unataka kazi hiyo hapo $1.80/siku hutaki - ondoka!"
Je hii inaweza kuwa "fungulia mbwa" ya mabiashara ya nje kugeuza Tz mahali pa kupatia a cheap labor force? Nini matokeo ya hiyo?

Je unadhani swala la uswahili (soma uafrika) linaenea hapa?.. I mean unadhani m-ndengereko mwenzetu angelipa zaidi kidogo kuliko $1.80? (Kama sikosei A-Z inamilikiwa na familia ya kihindi - not that there is anything wrong with that.. lakini... mhhh... $1.80 kwa jasho la siku jamani?)

Talk to me!
Ned

Friday, July 14, 2006

Attitude zetu na maendeleo ya nchi

*Nashukuru kwa mlioniandikia comments na maswali kwenye email binafsi, nitawasiliana nanyi – binafsi)
===
Leo nitajaribu kuelezea kidogo kile ninachoona kama sababu mojawapo zinazochangia hali mbaya ya wananchi wa kawaida – na nafasi iliyopo kubadili hali ilivyo.
*samahani ni maelezo marefu kidogo...
===

Pamoja na kuwa kuna kila dalili kuwa hali ya uchumi nyumbani imebadilika (na takwimu zinaonyesha hivyo), bado badiliko hili halitafsiriki katika badiliko la hali ya mwananchi wa kawaida.
Mojawapo ya kinachosababisha hali hii ni ukweli kuwa; sehemu kubwa ya mabadiliko ni ongezeko la pato la serikali; - sehemu kubwa ikiwa inatokana na ongezeko la pato toka kwenye utajiri wetu wa ardhini (madini, utalii n.k) - foreign direct investment (FDI). Yaani pato limeongezeka kutokana na fedha zilizozalishwa kwa fedha toka nje ya nchi.
Mapato haya moja kwa moja yanatunisha mfuko wa serikali – lakini unless ongezeko ni kubwa sana kwa muda mfupi, ni nadra sana kwa ongezeko kama hili kuwa na immediate impact kwa mwananchi wa kawaida. This is how it works:
Mwekezaji anakuja, anachimba madini… analipa tax, royalties na vikorombwezo vingine. Generally serikali itatumia pato ililolipata kujaribu kuendeleza miundombinu (infrastructures) ili kujaribu kuvutia wawekezaji zaidi. Wakati ambapo matumizi kama haya si mabaya – na mara nyingi muhimu, si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuona faida yake moja kwa moja – Why? Kwa sababu, mwananchi huyu bado ni maskini na anachohitaji ni ongezeko la moja kwa moja la pato lake binafsi – kuliko anavyohitaji kuona barabara mpya ya lami imejengwa!

Unaweza kudai kuwa uwepo wa wafadhili hawa unaongeza ajira – kweli; lakini naweza kukujibu kuwa ongezeko hili ni dogo kuliko tone la mvua katika bahari. Why… sana sana mwekezaji ataajiri watu… say 2000 kwa ajili ya mgodi, + watu kama 8000 wengine ambao watafaidika kwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na uzalishaji unaoendelea… top kiasi takribani watu kati ya 5,000 – 10,000 watafaidika. Tatizo ni kuwa, wengi ya watakao faidika ni wale wanaoishi maeneo yaliyo karibu na shughuli za uzalishaji – say Mwadui! Wengine walio mbali… say Pemba & Kisarawe watakachoambulia ni pale serikali itakapokuja kujenga barabara, shule au hospitali – na hata hili wakati mwingine ni kwa manati – kutegemea kama hiyo sehemu ina-potential ya kuvutia wawekezaji zaidi.

Wakati huo huo hao watu wa Pemba/Kisarawe – hawana kazi, mavuno shambani shida, na hawana kipato hata cha kulisha familia yao. Katika hali kama hii, ni rahisi sana kwa watu kulalamika. Why?... kwa sababu watu wanaona na kusikia mabilioni yaliyo patikana kutokana na wawekezaji, wanaona wenzao wa sehemu nyingine wanatanua (yes siku hizi wenye navyo ni matanuzi bila aibu… bila kujua wana waumiza sana mioyo wasio nacho), na kama vile kutia chumvi kwenye kidonda, baadhi ya viongozi tuliodhani wapo kutetea maslahi yetu, wanafanya mambo ambayo yanatia uchungu. (By the way, ninaamini hii ni moja ya sababu kubwa ya kuwepo kile kinachojulikana kama “the curse of oil/gold” – Yaani kuwepo kwa vita sehemu nyingi zenye utajiri wa mafuta na dhahabu – topic tofauti)

Back to Tz:
Kwa kuwa tatizo kubwa lipo kwenye pato binafsi kuwa dogo sana, ni dhahiri kuwa jibu (solution) ya maendeleo ya kweli yatakayoweza kuleta mabadiliko katika hali ya mwananchi wa kawaida, lipo katika kutafuta na kupata njia ya mwananchi huyo kuongeza kipato chake binafsi. Hii ni ili mwananchi huyo aweze:
- Kukidhi mahitaji ya familia yake (Chakula, malazi & mavazi, + shule kwa watoto) NA,
- Kuwa na kiasi cha ziada ambacho ataweza kukitumia kwa jinsi atakavyopenda (disposable income)
Ongezeko la kipato cha mtu wa kawaida NI LAZIMA iwe a priority… nina amini unless ongezeko hili linakuwa a reality, hali itabaki kama ilivyo.

Nini kifanyike?
Nadhani La muhimu kabisa ni kwa sisi waTz – kama jumuia NZIMA; kubadili namna tunavyo yatazama maisha yetu (A total overhaul of our attitudes as a society).
Now, kuna baadhi yetu tunaona kama wanao tuangusha ni viongozi wetu… kuna ukweli kidogo katika hilo…Kuna baadhi ya viongozi… (kunradhi ashakumu si matusi), kwa kweli have no business leading anybody! Hata hivyo ni lazima tukubali ukweli kuwa, ni makosa kudhani kuwa 100% ya matatizo tuliyonayo kama jumuia ni viongozi. Aidha, ni muhimu kukumbuka kuwa viongozi wametoka miongoni mwetu! Yes, kuna baadhi yao mizebwe (for lack of a better term)… lakini tunachokiona ni a sample ya tulivyo kama jumuia! Tatizo letu ni la ki-jumuia! Ndio maana utaona kana kama kila anayeingia kwenye uongozi – bila kujali kama ni mgeni au la, mpinzani au CCM, - inakuwa kama mtu umelogwa vile! Jibu ni… wote wanatoka from the same piece of cloth that we came from.
So ili hali ibadilike ni lazima kama jumuia tubadilishe our ATITTUDES!
(*hivi Kiswahili cha attitude ni nini?)

Sasa kuna facts zinazoandamana na attitudes, mfano:
- attitude si kitu cha kuzaliwa, ni kitu tunachojifunza kutokana na mawiwa (experiences) + mazingira tuliyonayo.
- attitude inaweza kuwa mojawapo ya aina mbili (2) tu! Favorable au unfavorable! Hakuna attitude za kati!
- Na, attitude ni matokeo ya kile tunachodhani au kuamini kama ukweli wa jinsi mambo yalivyo (our perceptions).
- Attitude determines behavior: Favorable attitude will bring about supporting and nurturing behavior while unfavorable attitude will bring about behavior which a less wanted. Mfano:
Inawezekana kutokana na nilichokifanya huko nyuma, ukawa unaamini kuwa mimi ni mtu mbaya kabisa. Imani hiyo, itapelekea kwa wewe kuwa na attitude ambayo ni unfavorable kuhusu mimi, na matokeo ni kwa wewe kuwa na tabia ya aina fulani mbele yangu – au ukisikia watu wananizungumzia.
Ukimwona mtu ana behave namna Fulani, jaribu kuchunguza attitude zake, na muhimu zaidi jaribu kuchunguza anachojua kama ukweli (anachoelewa – perception yake) kuhusu kinachojadiliwa.
Kwa maneno mengine, tabia kama
- kunung’unika (na rahisi zaidi kutafuta mtu wa kumlaumu)
- tabia tegemezi ya kusubiri hadi mtu baki aje atusaidie (au vizuri zaidi kutafuta mtu wa kumlalia – rushwa etc)
- Kukata tamaa – na kubweteka bila hata kujaribu kutafuta majibu ya matatizo
- kuamini kuwa kuna njia rahisi ya kuondokana na matatizo yanayotukabili au hata kutajirika (a short cut) n.k.
ni matokeo ya attitude zetu kuhusu maisha na namna tunavyoweza kufanikiwa katika maisha!

Sasa iwapo ni kweli tunajifunza attitude tulizonazo, kuna namna na nafasi ya kujifunza attitude zitakazotuwezesha ku-behave in a manner that will support our desire to develop as a people.
Ukweli huu ndio ulionifanya nidai (in a way) katika mada yangu iliyopita kuwa, wasomi, na tulio bahatika kutoka nje ya nchi na kusafisha macho, we are obligated to find ways that will change the way things are done back home.
- Tupo kwenye mazingira tofauti,
- Tunaona wenzetu wanavyotazama maisha
- Wenyewe tumejifunza ku-survive na kuona maisha kama wao
(believe me sio rahisi kuingia kwenye jamii tofauti na – sio tu kujifunza wanavyoishi, bali na ku excel)
Kwa maneno mengine: nafasi ya kutoka nje, inatupa exposure tofauti ambayo kwa namna moja au nyingine, na penda tusipende, itakuwa imebadilisha our perceptions.

Niishie hapa kwa leo… talk to me!
Ned

Friday, July 07, 2006

Wasomi, attitude zetu na maendeleo ya Tanzania

Bila shaka ushaona taarifa za hivi karibuni za Tanzania kupewa msaada wa $38 million, kwa ajili ya ujenzi wa barabara...hasa zinazounganisha Dar – Mwanza.
Unaweza kusoma sehemu ya taarifa hiyo hapa

Taarifa hiyo pia imeweka wazi ukweli kuwa, tangu 2002 EU imeshatoa kiasi kama $216 millioni kwa barabara za Tanzania, na kuwa kudai kuwa, pamoja na misaada hiyo bado barabara za Tanzania zina hali mbaya … nikiwanukuu “…Despite these efforts, Tanzania's road network remained primitive and quite limited, even by African standards…”
Swali kubwa hapa ni: "Iwapo dola millioni 216 kwa miaka 4; hazikuleta tofauti kubwa, tutegemee nini kutokana na hizi milioni 38 tunazopewa?

Naomba ieleweke kuwa kama mTz, msaada wowote unakaribishwa.. kwa mikono yote miwili.
Yes, nipe millioni leo.. guarantee nina uwezo wa kutumia every senti na wala sinta ugua moyoni:) So msaada?... bring it on!
Lakini kama mTz pia ni wajibu wangu kuweka wazi wasiwasi wanug wa namna tunavyotumia hii misaada tunayopata.
Ukweli waunguana ni kuwa, huu urahisi wa kupata misaada hautaendelea kuwepo milele. Aidha misaada kama hii mara nyingi huwa na gharama - kama kupoteza utu wako, + manyanyaso ya hapa na pale. Kama huamini, jaribu kumruhusu mwanaume mwenzako aanze kulisha familia yako uone kitakachotokea!

Kama watu huru, NI LAZIMA tufikirie namna ya kijunasua toka kwenye utegemezi huu... huko kwetu kuna methali isemayo "mtegemea cha nduguye hufa maskini..."
Regardless of your political view, ni ukweli ulio wazi kuwa NI LAZIMA ifike mahali tuweze kujitegema katika mambo kama haya
Mfano mzuri upo hata kwenye hiyo article: Mwandishi kwa kweli katuweka uchi vibaya sana... ati barabara zetu ni very primitive - Hivi kweli ilikuwa ni lazima aweke hiyo statement? Sidhani kama tuna jibu... lakini inawezekana it was simply a matter ya kujionyesha duniani kama EU wana "roho nzuri" sana ya kusaidia - masikini wenye barabra zilizo "primitive" sidhani kama ni... Dhalili kama hizi kwa kweli haziniingii moyoni kabisa - badala yake zinanitia hasira tu!

Swali ni; nini inabidi kibadilike Tanzania?
Awali kabisa: Ipo haja ya kubadilisha attitude zetu kuhusu maendeleo. Inaelekea wengi tupo tupo tu... tunasubiri maendeleo - na hii ni kutoka viongozi hadi mzee kule kijijini. Ukweli ni kuwa; maendeleo yoyote yale, hayaji automatically... Hayaji kwa kuwa una dhahabu nyingi ardhini, au mafuta au amani au - whatever else ulichonacho. Maendeleo huja pale mtu unapokuwa tayari kukaa chini na kufikiria kwa kina - kuhusu namna ya kutumia resources ulizo nazo kujiinua toka ulipo. Hii misaada ije tu... lakini hatuwezi kuendelea kuitegemea forever!
Katika kusema hayo - what do we have (tuna nini)?
Tanzania imekuwa ikisomesha watu tangu miaka ya 60! Wengi wapo sehemu mbali mbali duniani ambapo - pamoja na kuwa huko nyumbani walidhaniwa kutokuwa very productive (kwa sababu yoyote ile) huku ughaibuni - wana shaini vibaya sana! Huku ughaibuni ni maprofessors, ma-engineers, wa vitu kama videophone na gadgets nyingine ulimwengu unazozitegemea, wachumi wanaotegemewa, ma-executives kwenye makampuni makubwa (ya wenzetu)... and the list goes on and on! - Swali ni namna gani tunawatumia hawa watu?
Tanzania inabidi kuwe na namna ambayo tutaweza kukinga ujuzi wa hawa watu wetu kwa faida ya nchi - the most logical thing ingekuwa kwa serikali ku-weka mkakati wa namna ya ku-tap hawa watu.
Sasa, huenda serikali haioni umuhimu wa even kuweka kitengo maalumu cha kujaribu kuvuna "brain power" za hawa watu... La muhimu ni kufahamu kuwa IPO HAJA ya kuwa na namna ya kuvuna huo ujuzi!

Kwa sisi wasomi/wakali (intellectuals) wa Tanzania... popote duniani: IPO HAJA ya sisi (yes ninajiweka katika kundi hilo) kuona umuhimu wa kutafuta namna ya kutumia ujuzi tulioupata huku ughaibuni kwa faida ya nchi. Kweli hakuna namna (hata kama mtu ungetaka) ya kuweza ku-share ujuzi wako hivi sasa -0 or at least hiyo namna hatuifahamu; na huenda ni kweli jamaa huko bongo (viongozi) haonyeshi kama wanatuhitaji... Ukweli wa mambo ni... Who cares?
Pamoja na sababu zote hizo, Why not trying to come up with a way of expressing our knowledge on how things should be run backhome?
- Hii ni kitu ambayo imekuwa moyoni mwangu kwa muda mrefu sasa... tangu mwaka jana (2005) nimenunua a hosting space, nina domain name... lengo lilikuwa nikujaribu kutengeza something like a "Think tank" made primarily kwa waBongo wanaoishi nje ya Tz... it has been a year,nimejaribu kutafuta mtu wa kusaidia kutengeneza at least a website for that kind of a thing... in vain. Kila mtu yupo busy. Kuna uwezekano wa kutafuta mtu na kumlipa.. but you know what.. I got other use for the few bucks in my pocket right now. Kuna host na kuna a domain name.. all paid for... anyone to help create this thing?

Ninachosema ni, we need to change! kama kweli tunataka Tz ibadilike, inabidi wote; Viongozi, wasomi na waTz inbidi tuwe na "usongo" na maendeleo - kiasi unakosa usingizi usiku! We are not there yet! Tunaona hali mbaya, tunalalama tu... Solution? no one gives one!
Ukwlei ni kuwa it really does not take a nabii au a genius kuona matatizo.. that is not a talent!... lakini it takes a special kind of a person to see a solution... and a genius to see the opportunity"

Nitoe mfano kwa kutumia hizo hizo barabara:
Tanzania... ukiona mkandarasi anapewa tenda ya kujenga barabara.. most likely ni ujenzi wa lami tu - hapo magari yanapopita oNLY!
Lakini inafahamika kuwa Tanzania takribani asilimia 95 ya watumiaji wote wa barabara ni watembea kwa miguu na wenye baiskeli! Hivi ni akili gani inayotushauri kuwa ujenzi ni kujenga lami tu wakati hao watembea kwa miguu (walio wengi) wanapita kwenye vumbi na kutengeneza vumbi zaidi (binadamu ni agent wa mmomonyoko wa ardhi). matokeo ni gari likipita vumbi mtindo mmoja! Wenye nacho wanafunga madirisha ya magari yao na ku-enjoy kiyoyozi! wavuja jasho inabidi kubana pua na kufunga macho (au kuinama kujaribu kukwepa vumbi!) Swali ni kwa nini hali hii?

Hapa kwa wenzetu, ukisikia mkandarasi kapewa tenda ya ujenzi wa barabara maana yake ni:lami (hapo gari linapopita) + sehemu ya watembea kwa miguu (yenye usalama) + taa za barabarani, + ishara za barabarani (zinazoeleweka) + miti na ukoka unao cover meter 10 za uwazi.

Swali kwetu ni - kwa nini hawa makandarasi wanapokuja kwetu wanajitia hawajuia standards za barabaraba? na kwetu wabongo, kwa nini tunakubali kuliwa na kujenga barabara "koko"?
Inabidi tuinue standard zeti na kudai standards zilizo sawa au bora zaidi kuliko zilizopo huku ulaya! Iwapo tutabadilika na kuanza KUDAI standard hizo, makandarasi itabidi wajiinue kuifikia - wanataka hiyo tenda vibaya sana - believe me! Lakini iwpao tutaendelea kujiwekea standard ndogo.. jamaa wataendelea kutanua - profits 100x - wengine sisi "kalang'hbaho"!
Ok unaweza kusema kuna mtu huko kwenye ulaji anakula 10%... Unajua binafsi nionavyo, iwapo sijui kuhusu hilo, na kama wananchi tunapata a good thing out of that contract... I trully do not care! (hata hapa US watu wanalamba hiyo 10% - wakati mwingine even more); tatizo ni pale ulaji wa hiyo 10% inaposababisha mtu unakuwa zebwe! halafu unajaribukutufanya sisi wengine wote mazebwe wenzako! hapo nina taabu na hilo. Swali kwetu ni... ni namna gani tunawawajibisha watu kama hawa? Au ndio kuwasifia... "...jamaaa bwana... katumia vizuri nafasi yake"... katumia nafasi yake kwa kifo changu...? waBongo inabidi tuwe wakali kwa hawa watu -na ikiwezekana kushinikiza watiwe lupango nakufilisiwa mali zao zote! Adhabu ni lazima iwe kubwa!

- Kwa kutokuwa na a meaningful way ya kuwawajibisha hawa mazebwe, tunajikuta hata usimamizi wa hizo kontrakti - unakuwa shida.
Aidha, Kontrakti ni makubaliano ya kibiashara: ina vitu muhimu ikiwa ni pamoja na gharama, style ya ujenzi na muda wa ujenzi huo kumalizika. Kila ujenzi unavyokawia kumalizika, ndivyo gharama zinavyoongezeka, na mara nyingi ndivyo ubora unavyopungua. Kwa nini tunaruhusu mkandarasi ku-get out easily wakati hawatimizi wajibu wao? Kuacha natural causes - ambazo hazizuiliki, Kwa nini tunakubali kupoteza muda, + kujitwika gharama za ziada kwa ajili ya ucheleweshaji? KWa nini mkandarasi asi TULIPE kwa kuchelewa kumaliza kazi yake?(Since we are not benefiting from what we have already paid for… we have to be compensated for the economic loss of use)
Mfano barabara ya shekilango... nani kawajibishwa kwa kilichotokea? Au ndo hivo lishapita?

Well.. naona niishie hapa.
38million dollars - zinakuja. Lakini tusipobadilisha mtizamo wetu kwa ujumla, tusitegemee chochote cha ajabu! Matokeo = loopholes, na watu kujipatia ulaji
* talk to me

ned