Katika gazeti la "The New York Times" la jumapili iliyopita (july 16), mwandishi - Daniel Gross alimnukuu MS. Jacqueline Novogratz (mmojawapo wa vingunge wa Rockfellar foundation na mshauri wa Bank ya dunia) akisifia kiwanda cha A - Z kilichopo Arusha kama mfano wa kuigwa katika juhudi za kuondoa umasikini. Unaweza kusoma taarifa hiyo hapa
Inasemekana, baada ya kupata mkopo wa $350,000 (420million Tsh), toka kwa mfadhili wa huku US, kiwanda hicho kimeajiri takribani wanawake 2000 ambao kinawalipa kama $1.80 kwa siku kuzalisha vyandarua vyenye dawa. Mama huyo alisikika akifagilia A-Z kama mfano wa kuigwa kuondoa umasikini...
Swali langu ni... unakubaliana na analysis yake?
Hebu tujaribu kupiga vi-namba kidogo!
Assuming kuwa watu hawa watafanya kazi kwa siku kama 23 kwa mwezi, $1.80 kwa siku inakupa kama $41.4 kwa mwezi. Ukichukulia wastani wa x-change rate ya TSh 1200/= kwa $, wakina mama hawa wanapata kama TSh 49,680/= kwa mwezi.
Kima cha chini Tz ni Tsh 45,000/= kwa mwezi (nirekebisheni kama nimekosea), na wengi "walioajiriwa" wanapata zaidi ya hiyo mara kadhaa!
Kwa upande mwingine...A-Z inasaidia! Inasemekana kuwa Tz pamoja na kuwa na a workforce of about 19.22 million people, ina unemployment rate ya kama asilimia 36 (36%)... yaani takribani watu 6.9 million (ambao wana uweao wa kufanya kazi) hawana kazi! A-Z inaajiri watu 2000 (0.03% ya wasio na kazi... kidogo lakini do hivyo; "chururu si ndo ndo ndo":)
Swali langu ni... unadhani katika rate ya $1.80 kwa siku tutafika? Au ndo hivyo tena... "unataka kazi hiyo hapo $1.80/siku hutaki - ondoka!"
Je hii inaweza kuwa "fungulia mbwa" ya mabiashara ya nje kugeuza Tz mahali pa kupatia a cheap labor force? Nini matokeo ya hiyo?
Je unadhani swala la uswahili (soma uafrika) linaenea hapa?.. I mean unadhani m-ndengereko mwenzetu angelipa zaidi kidogo kuliko $1.80? (Kama sikosei A-Z inamilikiwa na familia ya kihindi - not that there is anything wrong with that.. lakini... mhhh... $1.80 kwa jasho la siku jamani?)
Talk to me!
Ned
0 comments:
Post a Comment