Monday, May 01, 2006

"Uwazi" na "Ukweli" na Mikataba ya uwekezaji

Miezi michache iliyopita, wengi tulifurahishwa na nia ya Mhe. raisi JK (na serikali ya awamu mpya), kupitia na kufanya tafhmini ya mikataba ya ubia na hasa ile inayohusu uchimbaji madini na raslimali nyingine.
Kwa walio wengi hizi ni taarifa za kutia moyo. Bado hatujafahamu hatima ya nia hiyo… na wengi bado tunasubiri tuone kitakachotokea.

Nimeona nizungumzie kidogo hili swala la "ukweli" na "uwazi" kwenye mikataba na wawekezaji: Ni kwa nini swala hili ni muhimu kwa mwananchi wa kawaida?

Dhana (perceptions)ya mwananchi wa kawaida:
Kwa kupitia lensi ya mwananchi wa kawaida kuna mambo yanayokubalika kama ukweli:
Ukweli #1: Maliasili za ardhini (madini, mafuta, gas n.k) zina thamani kubwa na kuwa nazo ni utajiri wa kutosha.
Hii haiitaji maelezo. NI ukweli ulio wazi kuwa hivyo ndivyo ilivyo. Hii inaweza kuelezewa na ukweli kuwa raslimali kama hizo ni chache sana. Si kila mtu/nchi inazo na inavyoelekea, kila mtu anahitaji kuwazitumia kwa namna moja au nyingine. Ukichukulia nadharia ya uzalishaji na mahitaji (supply and demand) utaona si "uchawi" kufahamu kuwa raslimali hizo ni utajiri. Kwa upande mwingine, wengi tunafahamu jinsi nchi yetu ilivyo masikini na jinsi umasikini huo unavyoniathiri mimi na watoto wangu. Ufahamu kuwa tuna madini - ambayo ni ya thamani kubwa; na kuwa tushaanza kuyavuna - unapelekea kujengwa kwa tumain kuwa... si siku nyingi "umaskini tulio nao utaondoka". Umasikini unauma! na ukweli ni kuwa hakuna masikini anayependa hali aliyonayo. Kila masikini ana tumaini la hali kubadilika siku moja. Inapotokea kuwa sasa tunajua tuna mali nyingi, tumaini na mategemeo ya "kuukata" yanapaa hewani! Tatizo la matumaini ni kuwa yasipotimilizwa.. matokeo ni kero (frustrations) - Hasa kama mtu huoni sababu za msingi zinazoweza kuzuia utimilifu wa matumaini hayo. Mara nyingi iwapo mtu atafahamu kinachopinga utilimilifu wa matumaini hayo - mara nyingi huwa ni rahisi zaidi kuvumilia na kuendelea kusubiri. Tatizo ni kuwa - kutokuwepo kwa maelezo mazuri ya sababu za kutokutimia kwa matumaini hayo kunaweza kuleta mtafaruku usiop wa kawaida.
Tatizo linakuwa baya zaidi, hasa kwa kuwa, kikawaida, sio wananchi walio wengi wenye ufahamu wa undani (details) kinachotakiwa kufanywa kabla ya raslimali hizi hazijafikia hali ya kuweza kutumika. Ukweli ni kuwa wengi tunaona ncha za mfumo mzima wa uzalishaji. Tunaona mwanzoni (kwenye machimbo) na tunasikia au kuona mkiani(tunaposoma au kusikia bei na mahitaji katika soko la dunia). Mzee anayeishi pale karibu na Bulyanhulu, anaona ujenzi ukianza na kumalizika, huenda amesoma headline kwenye gazeti au kusikia kuwa serikali imeingia mkataba na kampuni “abc” kwa kiasi “123” kwa ajili ya shughuli anayoiona. Kila siku anaona kiasi cha udongo unaochimbwa - mara nyingi hakuna taarifa ya kiasi gani cha huo undongo ambacho ni madini... mzee anachoona ni “volume” kubwa ya udongo -na mawazoni mwake huo wote ni dhahabu! Aidha, huenda amesikia kwenye vyombo vya habari “bei ya dhahabu katika soko la dunia sasa imefika $ kadha wa kadha kwa uzio mmoja...”
Mzee anachofanya ni kukaa chini na kuanza kupiga hesabu kidogo. Nimeona udongo wote ule ...nadhani ni kama malori "kazaa"; zidisha mara $ kazaa... mama weee...“Mungu ibariki Tz...” - wimbo wa taifa unaimbwa kwa kikabila.
Ninachosema ni kuwa kukosekana kwa taarifa zaidi kunaweza kupelekea kwa mtu kuja na namba zisizo kweli. Kama ilivyo kwa mwanadamu mwingine yeyote yule, waTz tuna tendency ya kutumia info kidogo tulizonazo, kukaa chini na kujaribu kufanya hesabu ndogo ndogo ili kujaribu kutafsiri maana ya hizo taarifa chache kwa maisha yetu na watoto wetu. Poor info... will almost automatically leads to a wrong interpretation of things.
Mfano: mzee anaweza akapata jibu lake (2 + 2 = 4). Tatizo linaweza kuanza pale taarifa zinazotoka kwa wakuu wa serikali zinapokuw ahazikubaliani na hesabu nilizopiga. mfano... serikali inaweza kusema" ... katika ule udongo wote uliouona tumepata $3" - kwenye akili ya mzee anachosikia ni "2 +2 = 3! Of course hiyo haileti maana yoyote.
Iwapo serikali haitajitahidi kumwelewesha huyu mtu kuwa, hesabu iliyotumiaka ni 2 + 2 -1... tatizo linaweza kukua na kuwa baya kabisa. wengi tunaweza kudharau hako katofauti ka (-1) - na inawezekana kabisa tukajisemea... huyu mzee inabidi aelewe. Well, you may be right, lakini ukichukulia hesabu mzee aliyopiga yeye pia yupo sahihi. Jawabu la hii kero ni kwa serikali kuwa wazi zaidi kuhusu mambop yanavyokwenda.
Tunajua kuwa secta kama madini, mafuta n.k :
Kikawaida ina thamani kubwa sana - the magnitude of the revenue at stake here is simply astounding. Logic ya kawaida ni kuwa thamani ya mradi inavyokuwa kubwa – ndio uwezekano wa ulaji unavyoongezeka – why? Palipo na thamani kubwa, mtu unaweze “kunyonya” senti moja moja kimya kimya – bila mtu kujua - kwa muda mrefu sana - in the process ukawa tajiri wa kutupwa. Watu wanajua hivyo na hivyo, kitu chochote kitakacholeta utata... uwezekano ni kushuku kuwa kuna mtu anapata ulaji. na hakuna mtu anayependa mtu mwingine apate ulaji kwa kupita mgongo wake.
2. Kwa asili, Biashara zinayohusu mali asili kama madini, zinahusisha watu wachache sana. Idadi ya "players" huwa kwa kawaida ni ndogo. Nina maana kuwa; kuacha wakina Masanja walio huko shimoni, wachezaji wakuu katika zoezi zima ni wachache sana - (huwezi kulinganisha ni secta kama kilimo). Kiuchumi, hii ina maana kuwa sehemu ya jumuia ambayo inafahamu undani wa kinachoendelea ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watu ambao wanashauku ya kutaka kujua kinachoendelea. Kwa mawazo yangu, hii kwa sehemu kubwa inaelezea sababu ya wananchi walio wengi kudai kuwepo wazawa zaidi kwenye nafasi za madaraka katika mashirika haya ya wawekezaji. Ni hulka ya kibinadamu kumwamini zaidi ndugu yako kuliko mtu wa mbali – “damu nzito kuliko kisusio” kindof a logic:)
3. Ukweli #2: Biashara ya maliasili kama madini ni relatively more complicated Ukilinganisha biashara ya madini na biashara nyingine kama kilimo (au hata viwanda), Madini ina hatua nyingi kidogo. Wakati ambapo inawezekana kabisa kwa mkulima wa kawaida kuamua kiurahisi kuvuna mkungu wa ndizi toka shambani kwake na, kuweza kupata mlaji literally a few steps kutoka shambani kwake, ni tofauti kabisa inapokuja kwenye biashara ya madini. Mvunaji wa madini anaweza kuwa Bulyankulu, Tz; na mlaji wa mwisho akawa Ohio, Marekani! Na hapo katikati... hako kajiwe kamoja kanaweza kuwa kamepitia hatua kadhaa - na kila moja na gharama yake kabla hakifikia kuuzwa. Hilo linaweza kueleweka kirahisi - na kwa kweli sidhani kama kuna tatizo hapa. tatizo ni pale ambapo watu wanasikia kitu kutoka kwenye vyombo vya serikali, na taarifa hizo hazilingani na zile ambazo "wawekezaji" wanazitoa kwa wadau wao - kama mafanikio yao (faida waliyoipata kutokana na biashara wanayofanya na sisi). Ndio maana tamko la Mhe. raisi linatia moyo - watu wanapata hizi taarifa za haya makampuni. na kwenye taarifa zao wana-tamba kuwa wamepata faida kubwa sana - wakati ambapo mimi na watoto wangu tunakufa njaa! - hapo ndipo inakuwa ngumu kwa watu kuelewa.

Kwa ufupi ni kuwa watu wanashuku zaidi inapokuja kwenye kitu kama madini n.k has kwa kuwa biashara kama hizi zipo very prone to mismanagement & abuse. Kwa sehemu, ndio maana utaona sehemu nyingi zenye matatizo ya vita na uharamia ni sehemu zilizo matajiri kwa hizo non-renewable natural resources (hivi ni nini kiswahili cha hii “non-renewable natural resource” ni nini? - Aibu kubwa...Kiswahili kinaanza kunigonga vibaya mno) – tuendelee -

Cha kufanya.
Nionavyo, wakati huu ambapo serikali inafanya tathmini ya mikataba hiyo, huenda ni nafasi nzuri pia kujiuliza namna ambayo inaweza kuwa wazi zaidi kwa wananchi kuhusu mikataba tuliyoingia na wawekezaji wetu. Sasa, kuna uwezekano kabisa tathmini hiyo ikaonyesha kuwa; tayari kuna uwazi wa kutosha. Iwapo itakuwa hivyo, then itabidi kutafuta jibu ya swali la nyongeza linalohusu "kueleweka kwa ujumbe unaotolewa" Yaani: ni namna gani serikali inaweza kuwasiliana na wananchi katika namna ambayo mwananchi wa kawaida ataweza kuelewa zadi kinachoendelea.
Hii itasaidia sana kuondoa kutokuelewana na shuku ambazo huenda hata si za kweli. Ikumbukwe kuwa, watu wataendelea kutafuta maana kwa kutumia taarifa walizonazo kupata dhana (perceptions). Dhana hizi, zinaweza ziwe au zisiwe za kweli - lakini ni dhana zao. Na kwa asili, dhana yoyote (perception) ya kweli au isiyo ya kweli... ni "ukweli" kwa mwenye nayo! Huo ni ukweli hata kama hatupendi.

KWa upande mwingine, kuna ukweli wa kibiashara kuwa, haita kaa iwezekane kuweka wazi undani wote wa mkataba wa kibiashara. Kufanya hivyo, ni sawa na kujiua kibiashara – hilo nalifahamu. Lakini pamoja na ufahamu huo, bado kuna uwezekano kwa vipengele muhimu vya mikataba kuwekwa wazi zaidi kuwa wazi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Baadhi ya sehemu ambazo huenda ingesaidia kwa wananchi kuelewa zaidi kinachoendelea ni pamoja na:
- Mipango ya hifadhi ya mazingira na “sustainability” ya mali zilizopo - Tukichukulia ukweli kuwa madini – by and large – are a non-renewable resource (ikiisha imekwisha); Ni vipi tunahakikisha jamaa hawakwangui hadi ukoko ambao huenda ukasaidia kidogo na vizazi vijavyo? Yaani – ni kwa namna gani uzalishaji unafanywa kwa kutilia maanani mipango yetu ya muda mrefu na ya muda wa kati? Nionavyo mimi, woga wa walio wengi, unasababishwa na dhana kuwa, hawa jamaa wapo busy kuvuna kwa kasi, kwa kadri wanavyoweza bila kujali matokeo ya muda mrefu - na kuwa; wakimaliza kila kitu wataondoka na kutuachia balaa la mashimo matupu. Of course logic inanilazimisha kuamini kuwa serikali yoyote makini itakuwa ishalifikira hilo - na wala sina shaka. Tatizo ni iwapo mwananchi wa kawaida anaelewa hayo; na wajibu wake katika kuhakikisha hawa jamaa wanafuata makubaliano.

- Uwakilishi katika majadiliano ya mikataba – Wakati nafahamu walio wengi bado wana imani na serikali iliyopo (boy... kukubalika kwa asilimia 80 si masihara!); bado kuna ka-upepo kanakoashiria kutokuwa na imani sana na namna tunavyowakilishwa kwenye majadiliano haya muhimu. Itasadia sana iwapo kungekuwa na namna ya kufahamu watu, vikundi au mashirika yaliyohusika katika majadiliano ya mkataba. Naomba niweke wazi kuwa wengi hatupo interested kufahamu majina binafsi ya wahusika! – hainisaidii kitu kujua "Hussein Issa Ally" amehusika kwenye mazungumzo – ukweli ni kuwa hata sijali (I really do not care - I do not even know the dude!); Lakini ningependa kufahamu ni ofisi gani, idara gani, shirika gani lisilo la kiserikali vimehusika katika majadiliano hayo - na ni nini mchango wao katika majadiliano hayo. Kuna ukweli kuwa, "Aliyepo mezani ndie anayekula"; ili kufahamu kama nina hata kanafasi ka kufaidi kidogo, inabidi niridhike kuwa nimewakilishwa vizuri. Katika mapana zaidi, ningependa kufahamu iwapo wananchi wa sehemu husika wamehusishwa kwenye mazungumzo hayo na kwa kiasi gani. Kweli tumefahamishwa kuwa kampuni “abc” itajenga shule, barabara, n.k. Vyema kabisa... lakini pia tungependa kujua huo ujenzi ni sehemu gani ya faida itakayopatikana. Iwapo itakuwa ni sehemu ndogo sana; tufahamishwe mipango ya ziada kuhakikisha tunapata zaidi? Lengo ni kuhakikisha wananchi wanaridhika na "juhudi" za kupata as much faida as possible - ndivyo wafanyabiashara wazuri wanavyofikiria = you push for a maximized profit! Mfano... haiitaji mtu kuwa mchumi kufahamu kuwa kudai 3% tu kwa ajili ya madini "yetu" si deal nzuri. Binafsi ninaamini kuna namna ambayo tungeweza kupata zaidi. Bila kujitia mjuaji sana - of which I am really not! Hivi hakuna uwezekano wa kugawana faida - nusu nusu? Yaani jamaa watoe gharama zao za mashine na uendeshaji... hiyo faida 50-50! Inaweza kuwa ndoto... may be hata hakuna kitu kama hicho; lakini ningependa kufahamu kunalikuwa na mtaalamu aliyefikiria hilo. Hii inapelekea kwenye point inayofuata
- Uwazi zaidi kuhusu "terms" za mikataba – Kwa ufupi, mwananchi wa kawaida hana mahitaji mkubwa sana... wengi wanachotaka kujua ni iwapo kulikuwa na juhudi za kutosha kufanya terms kuwa as favorable kwetu as is practically possible. Of course mfanyabiashara yeyote (kama mwamba ngoma) atajaribu kuvutia kwake. Hii ni bila kujali kama tu-masikini au la. Inapofika katika majadiliano ya terms... we are on equal footing. "una kitu ninachokitaka, na mimi nina kitu unachokitaka!" Huji hapa kunisaidia - na wala si kwa sababu una roho nzuri sana ndio umekuja hapa - Wengi wa hawa wawekezaji wamekuja kwa sababu wanajua watafaidika - period. Sasa tuache kuchezeana akili na tuanze kujadiliana kama watu wazima.
Tunachotegemea ni kwa wawakilishi wetu kuwa wagumu kidogo kukubali terms ambazo kwa walio wengi zinaelekea kuwa “borderline upuuzi” terms ambazo hata wao wenyewe wasingezikubali kama kibao kingegeuzwa!

A big pat on the back!
Kuna dalili nzuri ambazo inabidi kuzishangilia. BInafsi, ninafurahishwa sana na jinsi serikali yetu inavyo lishughulikia swala la EU na uvuaji samaki! Hata mtoto mdogo angeweza kuona kuwa deal ya awali haikuwa nzuri kwetu! Pamoja na kuwa tunahitaji sana hiyo "Euro" ile deal haikuwa nzuri hata kidogo. Ukweli kuwa serikali imeliona hilo na kulifanyia kazi.. ni jamo la kusifiwa.
Sasa inaweza kufika mahali ikabidi kukubaliana nao katika namna ambayo pengine hatutapata kila kitu tulichotaka... but, then it should be the same to them! Boashara ni makubaliano. Unatoka huko uliko-ninatoka nilipo - tunakutana katikati! Bravo katika hilo!
==
NJia zinazoweza kusaidia:
1. Hamasisha ushiriki wa vikundi vya uwakilishi kwenye mazungumzo ya mikataba
Mojawapo ya njia ambazo serikali inaweza kutumia kuhakikisha haya makubaliano yanafanyika kwa uwazi zaidi; ni kujaribu kuhamasisha na kusaidia wananchi (hasa wa maeneo husika), kuunda vikundi vyao vya uwakilishi(kitu kama kamati ya wazee/walezi - what ever name), na kuhakikisha vikundi hivi vinapata nafasi kwenye meza ya majadiliano.
Hapo zamani kulikuwa na mawazo kuwa wananchi walio wengi hawataelewa kinachoendelea. Well, sio tu huu si ukweli wote - bali pia inabidi kuweza kuwahamasisha kuanza kujifikiria zaidi kimaendeleo kuliko kusubiri ajira tu!
Nionavyo mimi hii ni njia rahisi zaidi ya kujenga uaminifu. Trust is always earned! not a right! Yes tunaamini serikali... lakini inabidi kujitahidi kulinda that trust. and the best way ni kuhamasisha ushiriki zaidi. Aidha, serikali inaweza pia kujitoa katika kazi ya kuweka haya maswala wazi, kwa tengeneza mazingira ambapo vikundi au makampuni binafsi vitaweza (kuvutiwa) kufanya utafiti wao na kutoa taarifa zao hadharani. Iwapo hakuna cha kuficha – sioni kwa nini hii isiwe an open area – provided vikundi hivyo vinapewa a reasonable guidelines – to protect the business nature of the agreement.
* Sikufuatilia sana swala la "haki elimu" - lakini mwenzenu hadi leo sina uhakika nafahamu kosa lao lilikuwa nini. Kama swala lilikuwa ni kwa wao kukosoa makosa fulani ya kiutendaji... huenda kujaribu kuwafungia hakuna matokeo mazuri (kuna mtu anafahamu kilichoendelea anifahamishe?) - otherwise nilidhani kuwa na kitu kama hicho - only kwenye sekta ya madini - something like "haki madini":) ingesaidia

2. Weka wazi taarifa za Mavuno na Mapato kwa muhula (quarterly reports for the public). Hivi kweli haiwezekani kwa wizara husika (Nishati na Madini?) kuweka kwenye mtandao wake taarifa ya muhula kuhusu uzalishaji na mapato kutokana na madini? Je hiyo nayo ni siri ya kibiashara?
Nilipata nafasi ya kutembelea tovuti (webpage) ya Barrick Gold ambayo ni mmojawapo wa wawekezaji wetu. Si tu kuna taarifa ya mwaka n.k; bali pia kuna kuna haya:
“…At the time of acquisition in 1999, proven and probable mineral resources were approximately 3.6 million ounces of gold. At the end of 2005, Bulyanhulu had 10.7 million ounces of proven and probable gold reserves…” – yaani mambo yenda yakiongezeka; wanaendelea… “…Drill results to date indicate that grades improve at depth. The current reserves are concentrated on one reef but significant exploration potential has been identified on two other reefs on the property.
In 2005, the mine produced 311,000 ounces of gold at total cash costs of $358 per ounce…”

Swali ni kama hawa jamaa wanaweka taarifa kama hizi kwenye tovuti yao… ni kwa nini tusiweke kwenye tovuti yetu kwa Kiswahili na tafsiri yake katika lugha rahisi?

Mfano kinachotakiwa kurekebishwa.
Kwenye katikati ya miaka ya 90, Barrick Gold International waliweka kwenye “prospectus” yao taarifa za ugunduzi wa kiasi kikubwa cha madini sehemu inayoitwa Bulyanhulu huko Tz. Baadhi ya wabongo hapa US na huko Canada walipata hiyo “prospectus” ambayo lengo lilikuwa ni kuvutia watu wanunue hisa katika kampuni hiyo (kwa kupitia NY stock exchange & Toronto stock exchange). Kwa kuona kanafasi ka kufaidika kidogo, baadhi ya WaTz waliamua kuwasiliana na wawakilishi wetu huku ughaibuni, ilikujua kama hiyo information ni kweli au la – ili wajitutumue japo kununua hizo hisa kabla hazijapanda bei. Taarifa tulizopata hazikuwa za kutia moyo – infact “mzee” wetu alikataa katakata kama hizo info ni kweli na kudai kuwa hiyo ilikuwa ni geresha ya hiyo kampuni ili wauze hizo hisa. Well, wabongo tukalemaa! Hardly two years later – it became official – Yes, Bulyankulu is on! Nani muhusika mkuu – Barrick Gold! Their stock price went through the roof!
Kwa tulio wengi - that was an opportunity missed – big time! By the time Barrick Gold wanatangaza kupewa ruksa ya kuchimba eneo hilo (1999) tayari bei ya hisa zao ilishapanda Karibu maradufu – kwa wenzangu na mie ambao fedha zenyewe kichele… that was not good news.
Ni wazi kuwa tukio kama hili halikusaidia sana perception ya watu kuhusu uwazi katika maswala haya. Nafahamu kuna uwezekanokuwa Barrick walikuwa hawajawapa serikali taarifa rasmi kuhusu ugunduzi wao… na hivyo kumnyima “mzee” wetu uwezo wa ksema kisicho “official” position. Lakini kuna viswali vinavyokera – mfano: “Hivi kweli ilikuwa ngumu kiasi gani kwa serikali kutoa taarifa kuwa “kuna kampuni “abc” inafanya uchunguzi hapa na pale – whatever -… bado hatuna taarifa rasmi ya walichogundua… iwpao utafanya uamuzi wa kuwekeza, wekeza at your own risk” - would that have been enough? Isingesaidia kujenga uaminifu kati ya wananchi wa kawaida na serikali? By the way… ni mategemeo yangu kuwa jamaa wanapoonyesha nia ya kuwekeza nchini kwetu –tunakuwa na namna ya kuhakikisha wanachotuambia – Si vibaya kumchunguza your potential business partner kabla ya kuingia ubia naye – As a matter of fact that is considered a prudent action to take. Sina maana kuwa serikali haifanyi a background check – lakini jamaa wanatangaza kwa wadau wao – bila ya sisi kujua? Inakuwa ngumu kidogo kuamini. Mategemeo ni kuwa tunajaribu ku-monitor nyendo zao kuhakikisha wanachowakilisha kwetu ni sahihi. Na pia kuna ka ukweli kuwa; uamuzi wa kuweka taarifa kwenye “prospectus” – an official document – wakati ambapo hujamtaarifu partner wako – hiyo inaweza ku-amount to a serous breach of trust. Ukweli ni kuwa kwa wengi ilikuwa vigumu kukubali kuwa serikali ilikuwa haijui chochote kuhusu hiyo deal. Hii ilipelekea kuwa na viswali vya ziada ambavyo huenda visingetakiwa hata kutokea.

Kuna haja ya serikali kutafuta namna ya kuweka mikataba inayoingia na wawekezaji wazi zaidi. Tukitilia maanani umuhimu wa wananchi kuwa na imani na serikali yao, kuna faida kubwa kuhakikisha mambo yanawekwa wazi kwa kadri inavyowezekana. Mtu unaweza kuuliza - fedha za kufanya hivi zotatoka wapi; kwanza - ni halali kabisa kwa mwenyemali kufahamu mali yake inavyotumika; pili: Ni hekima kutumia sehemu kidogo ya mapato kufanya kitu kitakachojenga uaminifu. Kuna gharama ya kulipa ili uaminiwe... na ukweli ni kuwa "uwazi" na "ukweli" ni gharama ndogo sana ukilinganisha na faida kubwa inayoweza kupatikana kwa kuaminiwa.

Samahani kwa maelezo marefu - hata sina uhakika kama yanaeleweka - whatever the case - at least I tried:)

Ned

2 comments:

mwandani said...

Elimu bin Elimu.
Nafikiri umbeya ya kuzua mambo ni matokeo ya taarifa finyu au kutokuwepo kwa taarifa. Siyo makosa kwa jamii isiyo na taarifa kamili kuzua mambo, ndio binaadamu tulivyo.
Inapokuja suala la utajiri wa nchi mikataba si sawa kuwekwa wazi, kwa kila detail, hii ni katika biashara yoyote, la sivyo unakosa nafasi ya ku-bargain.
Ila kuna maelezo ya jumla ya mkataba. Ukiangalia Libya ilivyouza leseni za mafuta kwa India na Marekani hivi karibuni, au makampuni yalivyoanza kuchimba mafuta Mauritania - unaweza kuona mikataba inavyofikiwa.

Kibali cha kupeleleza na haki ya kuvuna au kuchimba mafuta - upfront wakati wa kuandika mkataba kinajulikana, mgawanyo wa mapato ya kuzalisha unawekwa wazi, siyo detailed lakini figures ziko wazi.

Mugabe (japo ana walakini) kaipitia tena mikataba ya madini na kaeleza mgawanyo wa mapato kati ya kampuni na serikali. Morales wa Bolivia anafanya hivyo hivi ninapoandika kuhusu mikataba ya uvunaji gesi.

Sidhani kama Tanzania itadhurika ikiweka picha wazi ya mikataba ya madini. Hatutaki nukta zote za makubaliano, nafikiri wengi wanataka kujua ili walinganishe kama tunaliwa au la?

Shukrani kwa kuchimbua kwa kituo juu ya hili.

mwandani said...

Nimepata kiungo:

http://mwandani.blogspot.com/2005/08/tujiponye-vipi.html

Niliwahi kugusia swala la kununua hisa wakati fulani huko nyuma kwenye kiungo hicho hapo juu. Nawe umezungumzia Barrck Gold. (by the way, hairuhusiwi kutaja dhambi za hii kampuni kama hauna wanasheria kama 100 wa kukukinga) Kuna mtu akanijibu kuwa hilo ni gumu kwa mtu aliyeko nyumbani, swala la kumwezesha aliyeko nyumbani ni la kipaumbele zaidi.

Inabidi tujifunze pamoja na mambo mengine utamaduni wa hawa jamaa, utamaduni wa kuwekeza, kucheza na benki, kucheza na hisa halafu kujenga capital assets.

Nimewatizama hawa jamaa kwa muda mrefu, hawana pesa wengi wao lakini wana mali - kivipi? Utamaduni wa kukopa - kila mtu ana mogeji, siye tunasubiri kudunduliza mpaka zijae. Wengi wana hisa sie tukiona hatupati faida kubwa kwa mpigo tunaona hailipi.Tujifunze kuwa na malengo ya muda mrefu na kushikiliya unaloamini. mtembelee blogu ya jeff Msangi kaandika juu ya kumaliza mbio... au kutokata tamaa.

samahani kwa maoni ya reja reja.