Friday, May 05, 2006

Moyo wa kujitolea - unahitaji kuchochewa

Wakati ambapo nina kila haki ya kujivunia ukweli kuwa Mungu katujalia Tz... pamoja na njaa kali iliyokumba maeneo ya A/mashariki na kati... nadhani Tz kidogo makali hayakuwa kama kwa wenzetu - atleast kwa kuchukulia taarifa mbalimbali tunazozipata. Serikali nyingi ziliweka hadharani vilio vya kuomba kusaidiwa; kwa tathmini ya haraka haraka ni wazi kuwa majirani zetu inakuwa ngumu sana kusikilizwa... wanasota hata kupata mtu wa kusikiliza kilio chao. Kwa mtazamaji wa kawaida, inaelekea Tz inaaminika zaidi kuliko wenzetu - na kilio chetu imekuwa rahisi zaidi kusikika na kupata misaada tuliyoomba. - that is good news (kufahamu kuwa ukiwa na shida marafiki watakuja kusaidia).
Waungwana, kujiweka katika nafasi hiyo ya kuaminiwa SI bahati. NI vyema kutoa sifa pale inapokuwa haki - na sina shaka wengi tutakubali kuwa juhudi za serikali yetu kujiweka katika mazingira ya kuaminiwa + juhudi za kukata makali ya njaa, zinastahili pongezi.

La kupendeza zaidi ni kuona cheche za moyo wa watu na mashirika binafsi kujitolea na kuchangia juhudi hizo. Si kwamba haijawahi kutokea Tz,lakini cheche hizo zimekuwa dhahiri zaidi wakati huu. Wahega walisema - "ushikwapo shikamana" NI jambo zuri kuona wabongo na sisi tunajaribu kufanya kila linalowzekana kujisaidia japo kidogo!
Wakati ambapo nafahamu sina sauti yoyote, nadhani haitakuwa mbaya nikitoa wazo... hasa hasa kwa tulio ughaibuni - kujaribu kuji-organize na kutafuta namna ya kujichangisha changisha - na kusaidia. Kutoa ni moyo...sio lazima mtu ujikunje mamilioni... chochte mtu ulichonacho kinaweza kusaidia sana. mafano kwa sisi tulio hapa US. Mtu mmoja akitoa $10, hizo ni kama Tsh 130,000/=; Iwapo watu kumi watajitutumua na kutoa hizo $10, 10...tayari kuna zaidi ya Tsh millioni moja na laki tatu! Hiyo ni kama mtu utaona $10 - that' all y can give. Iwapo utaamua ku-double that... kishindo chake ni kikubwa zaidi! Hata kama mtu utaamua kutoa kitu kidogo zaidi...(hebu tuseme... unaamua kutoa less than the price of a burger...) huko nyumbani hiyo $2-3 ni kitu kikubwa sana...utakuwa ume-serve watu kadhaa! Sababu ya kushauri kuji-organize, ni kwa sababu, wakati ambapo your $10 inaweza isilete tofauti sana (by the way, hiyo hata hailipi bei ya western union - kutuma fedha TZ -just a "freebie"); kukusanya nguvu za watu kadhaa, zinaweza kuleta tofauti kubwa.

Kuna faida ya ziada ya kutoa: Sio tu mtu unakuwa umeshiriki katika kitu ambacho utakuwa na haki kabisa ya kujivunia... pia, inajenga tabia ambayo kwa wenzetu tunaowaona wameendelea -imekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo yao; tabia ya kujitolea. Kila mwaka hapa US, fedha zinazopatikana kwa watu kujitolea ni mabilioni ya $$$. KWa kuwa mara nyingi fedha hizo zinatumika kwenye jumuia - Yes, wanaosaidiwa wanafaidika, lakini pia wanaotoa - wanafaidika katika namna ambayo si ya moja kwa moja (indirect benefits).
Wajibu wa serikali
Katika jumuia au nchi yoyote, serikali ina wajibu wa kutengeneza mazingira mazuri, kwa watu kufanya vitu vitakavyoleta maendeleo! Kwa upande wetu, serikali inaweza kuchangia sana katika kuhakikisha inajenga mazingira yanayoweza kuchochea moyo wa wa TZ kujitolea na kuchangia vitu vya maendeleo. Mf. hapa US ukitoa mchango wako kwa kitu ambacho kinafahamika kama maendeleo ya jamii, unapata kanafuu fulani katika kiwango cha kodi unayokatwa - tax deduction. Wakati ambapo mtu unaweza kujenga hoja kuwa hiyo inaweza ika-futa juhudi za serikali kukusanya kodi zaidi; ukweli ni kuwa serikali inapata faida zaidi kuwa na mfumo kama huo. NI kama kesi ya kuacha kuchukua Tsh 1/= ili upata Tsh 10/= baadaye - kuna faida. Hivyo si mbaya nikishauri kwa serikali (kwa kupitia bunge or otherwise) kufikiria namna ya kuhamasisha watu kujitolea zaidi.Inaweza kwua kwa kutunga vi-sheria ambavyo vitapunguza makali ya kodi - kwa kiasi kilichotolewa, au hata kupata namna ya ku"watambua" hadharani wale wanaojitolea.

(* note: nina "assume" hatuna visheria kama hivi -kama vipo samahani kwa kurudia kitu ambacho tayari kipo)>

kwa ufupi ni kwamba... iwapo tunaamini maendeleo yanaletwa na watu wenyewe, inabidi tuwe tayari kujitolea zaidi, na kw aserikali kuwa tayari kutafuta namna ya kujenga mazingira yatakayochochea moyo kama huo.
Ned

2 comments:

Jeff Msangi said...

Ned,
Nakubaliana kabisa na wewe kwamba kujitolea ni jambo muhimu sana kama tunataka kujenga taifa letu.Nchi hizi tunazoziita zilizoendelea zinajengwa kwa kiasi kikubwa na volunteers,kijamii,kisiasa na hata kiuchumi.
Labda kukurekebisha kidogo tu..dola 10 za kimarekani sio sawa na Tshs 130,000/=. Badala yake dola kumi ni sawa na Tshs 13!
Pia sheria unazozipendekeza za tax deduction zipo.Tatizo ni mfumo mzima wa kodi wa Tanzania bado haujatengemaa kwa sababu hata hivi sasa ni vigumu kujua nani analipa kodi na nani halipi.

Mshimo said...

Jeff ulikuwa na nia njema ya kusahihisha lakini na wewe kama ned umeenda to the extreme side. Dola 10 ni kama 13,000 sh na siyo 13! Sh yetu hajawa na thamani kiasi hicho cha kutofautiana kwa sh mbili tu. Na kwako ned ilikuwa na hiyo millioni inatakiwa watu 100 na siyo kumi