Wednesday, May 03, 2006

Mhe. raisi aunda tume ya kutathmini mikataba ya uchimbaji madini

Raisi ametimiza adhma yake ya kutathmini mikataba yote ya uchimbaji madini - kwa kuunda tume maalumu kwa shughuli hiyo. Unaweza kusoma taarifa hizo hapa
Wakati ambapo ni kweli kuwa huu ni mwanzo tu, kwa mwananchi wa kawaida taarifa hii ni ya kutia moyo sana - kuwa at least serikali inaonyesha kutilia maanani umuhimu wa wenye mali kuona faida za mali yao.
Nafahamu kwa baadhi ya wawekezaji... hii si taarifa nzuri. Lakini inabidi waelewe kuwa, Tz haina nia ya kuwafukuza au kuzuia wasifaidike na juhudi zao. Ni katika kuhakikisha hakuna anaye "mlalia" mwenzake - ndio biashara inavyotakiwa kuwa.
Iwapo haki inatendeka - hawana haja ya kuogopa lolote. Lakini kama mambo yenyewe ndio ya ki- "mkia wa fisi" - Yes, wana kila sababu ya matumbo kupata joto!
Hongera Mhe. raisi - mara nyingi inahitaji moyo kusimama kidete kwa hawa jamaa:)
Ned

0 comments: