Wednesday, May 17, 2006

Machinga (Hawkers) au sekta isiyo rasmi?

NIlikuwepo Dar kwenye mwezi wa tatu mwaka huu; na katika pita pita yangu, nilishuhudia askari wa jiji wakiwa kazini kuvunja vipanda vya wafanyabiashara wadogo pale karibu na kivukoni. Aidha kulikuwa na fununu kuwa jiji lilikuwa lina mpango wa kujaribu kuwashughulikia wamachinga ambao wameenea sana jijini.
Kwa upande mmoja; wamachinga wanatoa ajira kwa vijana - takribani asilimia 36 ambao hawana kazi Dar! Nilifanikiwa kumuhoji muuza mananasi mmoja ambaye alinifahamisha kuwa kwa siku anapata kama Tsh 5,000/= - na anafanya kazi siku 6 katika wiki (6 x 4) x 5,000 = Tsh 120,000/= mara 3 ya kima cha chini cha mshahara! (wakali wa namba nisahihisheni)
Kwa upande mwingine; kuna wanaodai kuwa wamachinga wanagh'asi watu, wengine ni wezi, na pia kwa kuwa mara nyingi wana-deal kwa cash, inakuwa ngumu kwa serikali kukusanya kodi ya mapato toka kwa wafanya biashara hawa (pamoja na kuwa nafahamu - na nilishaona watumishi wa jiji wakiwakatisha ka-kodi - nadhani ni ka usafi:)
Pia ninavyofahamu - kuwa kuna pande mbili zinazo-chochea uwepo wa machinga.
Kwa upande mmoja hawa wafanyabiashara wanajitafutia maisha kama mtu mwingine yeyote.
Kuna "influx" kubwa ya vijanakuja mjini - siwalauma kwani hata mimi ningefanya hivyo hivyo. Hii inatokea wakati ambapo kasi ya kubuni na kuanzisha ajira haiendani na kasi ya ujio wa vijana hawa
Pia vijana hawa wanapata faida kiasi - atl east wanapata zaidia kuliko kima cha chini! Il kufanikiwa zaidi, wanajua wapi watakapoweza kupata wateja wengi - kutokana na aina za biashara yao
Kw aupande wengine, wateja nao nia yao mmoja! Kupata bidhaa wanayoihitaji kwa bei poa kwa kadri itakavyowezekana! Mara nyingi bei za machinga ni poa kuliko za huko dukani.
Aidha

Maswali:
Hivi hii hali ya umachinga ni kwetu tu? - Wenzetu wanafanya je?
Ukitilia maanani kuwa wengi wana-deal kwa cash; ni namna gani serikali inakusanya kodi toka kwao? (kuacha kodi ya usafi inayotozwa na jiji)?
Ni nini dawa ya kudumu itakayoleta ushindi kwa kila upande (jiji vs vijana wa machinga) - win-win situation?
Ni nini jina sahihi: Mashinga au sekta isiyo rasmi?

Ned

4 comments:

mwandani said...

kwani machinga wanakata leseni na kulipa kodi au?
tofauti nadhani ni msamiati tu. ndiyo hiyo hiyo sekta isiyo rasmi.

Boniphace Makene said...

Ned suala la machinga linatakiwa kujadiliwa kwa kina kwa kutazama pande mbili za sarafu. Je unaamini hii ni kazi ambayo mtu anaweza kuifanya hadi kuzeeka au ni kazi inayoweza kumkuza mtu kiuchumi na kisha kuiacha na kwenda hatua ya pili au ni kimbilio la kukatisha njia ya kusaka maisha ya muda mfupi? Nini nafasi ya umma na serrikali hasa katika kujali kundi hili ambalo hasa ndilo linalohitaji serikali kulinyanyua kwa kuliwkea mikakati maridhawa ya kimaisha ili liweze kuwa na uzalishaji unaoendelea na unaorutubisha maisha ya watu hawa? Kuna mjadala mkali kuhusu hili kwa kweli.

ned said...

Mwandani - awali samahani, kidogo nilikuwa safarini na sikuweza kuwa na nafasi ya kukujibu (Pamoja na kuwa nilisoma posting yako mapema).
Sina uhakika kama machinga huwa wanakata leseni ya biashara kama biashara nyingine. Isipokuwa nafahamu kwa uhakika huwa wanalipishwa kinachoitwa "kodi ya usafi" na jiji. Kama sikosei wanalipishwa kodi hii wanapotokea mitaani.
nadhani kama kuna mtu anayefahamu utendaji wa jiji anaweza kutupa taarifa kamili zaidi.
Ned

ned said...

Makene,
nakubaliana na wewe kuwa swala la machinga linabidi kutafutiwa jibu.
Ukichukulia ukweli kuwa jiji kama Dar lina unemployment rate ya karibu asilimia 46; utaona kuwa secta isiyo rasmi (kama machinga ilivyo) inaweza kuwa jibu la matatizo ya wengi.
Lakini siamini kuwa machinga kama walivyo sasa wanaweza kuleta mabadiliko yoyote ya maana kwa jamii. (Note neno "ya maana"). kwanza kwa asili ya biashara yenyewe - itakuwa ngumu sana kwa serikali kuweza kuwakaba kwa ajili ya kuwalipisha kodi. Kwa sehemu- ndiyo maana wanaweza kuuza bidhaa zao kwa bei poa - hawana cha VAT wala kodi ya mapato. Ukichukulia kuwa uwezo wa serikali kutoa support inayohitajika kwa maendeleo inategemea kodi - sina uhakika wa mchango wa secta hii kwa hayo maendeleo.
Pili: Nadhani kuna machinga na machinga. Kuna ambao baada ya kukata mbuga kwa kipindi, wameweza kuwa "ajiri" wenzao. na hivyo wao wanakuwa kama "middle men". hao nadhani wanauwezo wa kupata kipato zaidi. Lakini si wengi wameweza kufanya hivyo.
NAdhani mojawapo ya mambo ambayo yangeweza kufanyika ni kujaribu kufanya utafiti wa asili na hulka ya biashara hii kwetu (Yes - zipo sehemu nyingi - hasa maeneo ya Asia; lakini kila sehemu asili na namna biashara hiyo inavyofanyika vinatofautiana kidogo).
Kisha - jiji kwa kufuata maoni ya wataalamu itafute namna ya kuwaweka sehemu moja na kuwapa support yote wanayohitaji. Kwa namna hii inawezekana hata wenye akili wengine wakawa tayari kuwauzia some sort of a retirement plan OR a healthcare package.
Kama serikali, nadhani itabidi ufanyike utafiti wa kina kabla ya kuparamia majibu kwa pupa.
Kuhusu umma - sina uhakika wa nini cha kufanya. Lakini kwa kweli sidhani kama ni haki kuwavunjia tu vibanda vyao - au kuwafukuza huko mitaani - bila kuwapa jibu la wapi wakimbilie kuweza kufanya biashara zao kwa amani na utulivu.
* Hebu fikiria; iwapo kusingekuwa na Kariakoo - unadhani wale wauza viungo wangeishia wapi? - Wengi tungewaona mitaani.
Nadhani Machinga ni sawa na hao kidogo. wapo mitaani kwa kuwa hakuna mahali maalumu ambapo wanajua nikienda hapo nitalindwa na sheria za nchi - ili niweze kufanya biashara kwa amani

Ned